Deuteronomy 6:1-6

Mpende Bwana Mwenyezi Mungu Wako

1Haya ndiyo maagizo, amri na sheria ambazo Bwana Mwenyezi Mungu wenu aliniagiza niwafundishe ninyi ili mpate kuyashika katika nchi ambayo ninyi mnavuka Yordani kuimiliki, 2 aili kwamba ninyi, watoto wenu na watoto wao baada yao wamche Bwana Mwenyezi Mungu wenu siku zote kwa kushika amri na maagizo yake yote ninayowapa, ili mweze kuyafurahia maisha marefu. 3 bSikia, ee Israeli, nawe uwe mwangalifu kutii ili upate kufanikiwa na kuongezeka sana katika nchi itiririkayo maziwa na asali, kama Bwana, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi ninyi.

4 cSikia, ee Israeli: Bwana Mwenyezi Mungu wako, Bwana ni mmoja. 5 dMpende Bwana Mwenyezi Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 6 eAmri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako.
Copyright information for SwhKC